Karibu Ubungo Christian Centre !

Tunakukaribisha kila siku ya Jumapili uabudu pamoja nasi. Lakini pia tunazo ibada na programu mbalimbali katika wiki nzima. Kama hauwezi kufika kanisani kwasababu moja ama nyingine , bado unaweza kushiliki kwa njia ya mtandao kupitia IBADA-Live!. Utaweza kuzishiliki ibada zetu moja kwa moja popote ulipo kwa njia ya intaneti.

Maono Yetu

Ubungo Christian Centre, kama sauti ya mtu aliaye nyikani, maono yetu ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kitaifa na kimataifa wakibatizwa katika Roho Mtakatifu huku tukiwa na ibada za kiroho, mafundisho halisi na sahihi ya neno la Mungu na hivyo kuzidi kuongezeka kama kanisa.

Mawasiliano

Ubungo Christian Centre tuko jijini Dar es Salaam, wilaya ya Kinondoni, karibu na Ubungo Plaza.

Simu: +255 756 771 537

Barua pepe: uccubungo@gmail.com

Misheni Yetu

Ubungo Christian Centre tupo kwa ajili ya kumuabudu Mungu katika Roho na kweli, katika kuuambia ulimwengu juu ya habari za Yesu na kuwapeleka waamini katika kumjua zaidi Yesu kupitia sifa, kuabudu na neno chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.