Ijue Misingi ya Imani ya kanisa la  Tanzania Assemblies of God

1.Tunaamini maandiko yamevuviwa na Mungu na hayana kasoro (2Tim 3:15-17).

2. Kuna Mungu mmoja wa kweli tu wa kweli aliyejifunua ktk nafsi tatu za Baba, Mwana na Roho Mt (kumb Tolati 6:4, Math 28:19).

3. Tunaamini Bwana Yesu ni mwana wa Mungu na ana sifa zote za Uungu( Yoh 8:58, 1Yoh 5:20).

4.Tunaamini Japo mwanadamu aliumbwa mkamilifu, hivi sasa ameanguka dhambini (mwanzo 1:26,27; 2:17, Rumi 5:12-19).

5. Tunaamini mtu yeyote anaweza kuokolewa kwa njia ya damu ya Yesu tu (Luka 24:47, Tito 2:11).

6. Tunaamini ubatizo wa maji mengi na ushirika mtakatifu ni maagizo ya Biblia yan Neno ( Marko 16:6, Rumi 6:4).

7. Tunaamini kujazwa Roho Mt kunafuatia kuokoka na kwamba vitu hivi viwili viko tofauti (luka 24:49, Matendo 1:4, 8).

8. Tunaamini ishara ya kwanza ya nje ya kujazwa Roho Mt ni kunena kwa lugha (2:4; 1Kor 12:4-10, 28).

9. Tunaamini mtu anapokea utakaso mara anapookoka (1Kor 6:11) na anaendelea kutakaswa maisha yake yote (Rumi 12:1,2; 1Thes 5:23).

10. Tunaamini Kanisa ni mwili wa Kristo (Efeso 1:22,23; 2:22).

11.Tunaamini Makusudi Ya Kanisa ni matano Kushuhudia (marko 16:15-20), kujengana (Efeso 4:11-13), Kuabudu (Yohana 4:23-24), Utumishi (1kor 12; Rumi 12),na ushirika (matendo 2:42-46).

12. Tunaamini Mungu anaponya wagonjwa na kila mwamini ana haki ya kuponywa (Isaya 53:4,5; Mathayo 8:16-17).

13. Tunaamini kufufuka na kunyakuliwa ndilo tumaini letu kuu lenye baraka (1Thes 4:16-17; Rumi 8:23, Tito 2:13; 1Kor 15:51,52).

14. Tunaamini Yesu Kristo atatawala ulimwengu pamoja na watakatifu kwa miaka elfu (zek 14:5; Math 24:27,30; Ufunuo 1:7; Ufu 19:11-14; Ufu 20:1-6).

15. Tunaamini Kutakuwepo na hukumu kuu ya mwisho (Math25:26; Marko 9:43-48; UFu 19:20; 20:11-15; Ufu 21:8).

16. Tunaamini Bwana ataumba mbingu mpya na nchi mpya ambamo ndani yake haki inakaa (2Petro 3:13; Ufu 21:22).