Maono ya TAG

Maono ya TAG, kama kanisa, ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kitaifa na kimataifa wakibatizwa katika Roho Mtakatifu huku tukiwa na ibada za kiroho, mafundisho halisi na sahihi ya neno la Mungu na hivyo kuongezeka makanisa. 

Misheni ya TAG

Tanzania Assemblies of God (TAG) ipo kwa ajili ya kumuabudu Mungu katika Roho na kweli, katika kuuambia ulimwengu juu ya habari za Yesu na kuwapeleka waamini katika kumjua zaidi Yesu kupitia sifa, kuabudu na neno chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. 

Maadili ya msingi ya TAG

Uaminifu Kibiblia, Uadilifu, Kuwajibika kijamii, Ushirikiano kama timu, Uvunaji kimkakati, Uwezeshaji wa uongoziUkuhani kwa waumini wote, Uwajibikaji wa usimamizi wa fedha, Ukuaji kimkakati, na Ubora.